Wednesday, April 6, 2011

KWELI UKOLONI MAMBO LEO UMETUSHIKA....LOL!!!!




NAZUNGUMZIA KATIKA SOKO TU.....SI MENGINE;
Nimekuwa nikijiuliza sana, kwanini Watanzania tulio wengi hata mimi mwenyewe wa kwanza kabisa.....tunapenda sana kushabikia na kushangilia sana timu za Ulaya, je wao wa Ulaya wanashabikia au kushangilia timu zetu?
Utakuta mtu mweusi kutoka kule Musoma amevaa jezi imeandikwa Chacharito, Rooney, Kakà...nk. Katika moja ya policy ya kuingiza ukoloni mamboleo ni kuwafanya watu weusi wadharau mambo yao....ni watu wachache sana wanaovaa jezi za timu kama; Yanga, Simba, Azam FC, Mtibwa....nk. Tuacheni utumwa jamani turudi nyumbani tuone namna ya kukuza soka letu la Tanzania.


No comments:

WATEMBELEAJI