Wednesday, April 6, 2011

NILIKUWA NAFUATILIA MJADALA FULANI WA BABU WA LOLIONDO!

Nilikutana na maoni ya watu mbalimbali kuhusu Babu Ambi wa huko Loliondo, nitaweka maoni baadhi tu, maana yapo mengi sana. Mjadala wenyewe ulikuwa hivi;
POPOBAWA, VIPARA, ALBINO AND NOW BABU WA SAMUNGE!
Watanzania tunahusudu sana ushirikina, tujaribu kujikumbusha matukio ya kishirikina yaliyowahi kutokea nchini; 1). POPOBAWA; Kuna kipindi ilisemekana kuwa kuna jini lilikuwa linawafanyia mchezo mbaya watu. 2). VIPARA; Wakati fulani watu wenye vipara waliuawa ikiaminika vichwa vyao vinaleta utajiri. 3). NGOZI; Mkoa wa Mbeya uliwahi kuwa na matendo ya uchunaji ngozi ambazo zilihusishwa na utajiri. 4). VIKONGWE; Maeneo ya Shinyanga, wanawake wazee wenye macho mekundu walituhumiwa kuwa wachawi hivyo walitafutwa na kupigwa mpaka mauti. 5). ALBINO; Ni mwaka jana tu! tatizo la mauaji ya walemavu wa ngozi ( ALBINO) walikuwa wanawindwa kama swala ikiaminika viungo vyao vinaleta utajiri. 6). BABU WA LOLIONDO/TIBA YA KIKOMBE; Muasisi wa tia ya magonjwa sugu kwa kutumia kikombe kimoja tu cha dawa. Kwasasa wanaibuka waganga mbalimbali wanaotoa tiba ya namna hii.
JE NCHI YETU NI YA WACHAWI AU BELIEVERS??
MAONI; - Babu wa Loliondo ni tofauti na hayo mengine na hawezi kabisa kufananishwa na hayo. Yeye haui mtu, wala habaki mtu.....anatoa kikombe cha dawa iliyooteshwa, na katika briefing zake anajaribu kutibu pia Roho. Kumlinganisha huyu na wauwaji ni kutokumtendea haki! hayo unayotaka yalinganishwe na Babu hufanyika kwa siri; lakini Babu mambo yake yote hadharani, hata mti anaotumia umeoteshwa pale nyumbani kwake;....si siri! Dawa inachemshwa hadharani na kugawiwa hadharani. Serikali inajikusanyia kipato kutokana na shughuli za Babu wa Loliondo, je uliwahi kuona serikali inakusanya ushuru kutokana na hayo mengine? JIBU;
Yaani hujasikia tu kama watu wamekufa?

No comments:

WATEMBELEAJI