Sunday, April 3, 2011

SALA NZURI KWAAJILI YA KWARESIMA HII...!!!

Ninakuungamia Mungu wangu mpendwa wangu, tazama najilaza miguuni kwako kwa majuto, ee Bwana ninakuomba unitazame kwa huruma, nalia...nahuzunika kwakuwa mimi ni mwenye dhambi. Ni mambo ya ovyo ovyo na upuuzi vinaniponza, kupenda mambo yasiyo faa...hasira, wivu, chuki, choyo na kiburi.

Ee Bwana ninakiri udhaifu wangu wote, unaujuwa wazi hata kama nikikudanganya, na sasa naona haya kwa dhambi nyingi nilizonazo, nachoka kuishi jinsi nilivyo....ninaona uchungu sana, unihurumie, unisamehe Bwana ninaumia na ninasikitika sana...hofu ni kubwa sana na mwili hauna nguvu. Popote nipitapo watu hunisema sana, ni wengi hunifyonza, hutikisa vichwa vyao, ni maisha gani haya tazama Bwana yanavyotisha sina mbele wala nyuma, mimi kweli ninashangaza. Tamaa za mwili ona zinavyo iangamiza roho yangu....adhabu inayokuja kwangu hakika ni ngumu sana kuitaja.

Ee Yesu ulikufa kwaajili yangu mimi, lakini ona sasa nilivyochanganyikiwa; si mtu, si mnyama ninasikitisha sana....wanyama, ndege, samaki na wadudu nao wananishangaa kwa dhambi nilizo nazo. Wanataka kunitega sijui sasa niende wapi ee Yesu wangu nihurumie, nisaidie Mwokozi wangu.

Ee Yesu ndiwe nguvu kwa wanyonge na dhaifu, nakuomba unigeuze niwe mtu mnyoofu, niungue mwili huu mwovu na kwa hasira utupwe mbali kabisa, ni maisha gani haya; taabu nyingi huzuni tele.....niwavute watu wengi wakufuate Mwokozi wangu, na mwisho nifike kwako kwenye furaha na uzima tele.
AMINA!

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

sala nzuri nimeipenda na nitaiweka kichwani mwangu. Baraka zake Mungu ziwe nawe kaka BARAKA

Baraka Chibiriti said...

Asante sana Dada Yasinta.

WATEMBELEAJI