Wednesday, April 6, 2011

TANZANIA.....AJALI AJALI AJALI: KILA KUKICHA KWANINI?





Barabarani Tanzania kila kukicha ni ajali tu!Huwa najiuliza sana hivi ni kwanini? Lakini napata jibu mwenyewe kabisa, kuwa; ni kutokuwa makini madereva wetu wakati wakiwa barabarani, kwenda spidi kali sana bila utaratibu kabisa, magari kuwa na matairi mabovu yanpasuka ovyo ovyo, magari mabovu bovu tu, lakini yapo barabarani kama kawaida, kuovateki ovyo ovyo...nk. Wakati barabara zetu ni finyu sana wakati mwingine ni bovu sana. Sasa nini kifanyike ili kusalimisha maisha ya watu, ambao wanakufa kila kukicha na ajali hizi?


Hizi picha nilipiga wakati nikielekea Dodoma, nikitoka Dar es salaam. Toka Dar hadi Dom, nilikutana na ajali nane (8) kwa siku moja tu! kati ya malori na mabasi yalikuwa yameanguka na mengine kugongana, yaani nilishangaa sana na kusikitika sana kwa ajali hizi, inaonyesha kabisa kuwa Watanzania vile hatujali umuhimu wa maisha kwa ujumla, tungekuwa tunajali, tungelikuwa waangalifu zaidi barabarani. Yaani ukisafiri barabarani unaogopa daima hujui nini kitakutokea, hadi raha ya safari inakuwa haipo kabisa.

No comments:

WATEMBELEAJI