Tuesday, September 13, 2011

SIKU NILIPOTINGA MJENGONI (BUNGENI) DODOMA - TANZANIA.














Likizo hii nimefanikiwa kuhudhulia Bunge mara 5 huko mjini Dodoma, na kujifunza mengi sana katika siasa....pia nilifanikiwa kukutana na Wabunge wengi sana na Mawaziri, katika kubadilishana mawazo mbalimbali. Nilipata nafasi ya kuongea na Waziri wa Mambo ya nje, Mh.Bernad Membe na kumwuliza maswali mbalimbali...likiwemo la uraia wa nchi mbili au zaidi katika nchi yetu, kwa niaba ya wenzangu wote Watanzania waishio nje. Kwakweli mazungumzo yalikuwa mazuri, na yeye mwenyewe Mh.Waziri Membe anasema analishughulikia swala hilo kwa ukaribu sana ili watanzania waishio nje wapate kupata haki zao ki sawasawa. Yeye binafsi alisema anasikitika sana kwa watu hasa viongozi mbalimbali wanao pinga sana swala hili. Na haoni sababu ni nini, aliniahidi sana kuwa atapigania sana mpaka tuwe na uraia wa nchi mbili.


-Nilifurahi sana tena sana kuongea na Waziri Membe kwa kirefu, pia kwa kunipa muda wake kuongea na mimi. Pia Jumapili moja nilikutana nae tena kwa mara nyingine Kanisani, Jimboni Dodoma kabla ya Ibada kuanza, pia tuliongea kidogo. Alinisisitizia kwa mara nyingine yupo mstari wa mbele na kuungana na Watanzania wote waishio nje ili wapate uraia, ili watetee haki zao msingi huko waishiko.


- Asante sana Mh.Waziri Membe kwa ukarimu wako, kukubali kukutana nami huko Mjengoni - Dodoma.






1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Ama kweli ulifanya mzunguko safi sana...

WATEMBELEAJI