Sunday, October 23, 2011

TAFSIRI YANGU KATIKA JUMAPILI HII YA LEO!

Ulivyosema tuache magugu na ngano, vikue pamoja tutavitenganisha baadae. Magugu yanasitawi, ngano inakonda......uturuhusu Baba twende shambani mwako tukang'oe magugu ili ngano istawi.
Mtu anakuja Kanisani anakusifu, anakuimbia.....huyo huyo ni kahaba. Yakitokea matatizo katika Jamii....anakuja na shehena kubwa ya misaada, watu wanamshukuru sana wakizani ni mcha Mungu sana, yule mtoa misaada....huyo huyo ni fisadi mkubwa!
Wapo waimbaji makanisani wanaokuimbia, wanaimba na kutafakari neno lako lakini wamefunikwa na haya magugu.....ungeyang'oa magugu waimbaji waonekane!

No comments:

WATEMBELEAJI