NGOMA AFRICA BAND NA NYIMBO MPYA ZA MIAKA 50 YA UHURU.
Bendi maarufu ya Muziki wa dansi Barani Ulaya ''NGOMA AFRICA BAND'' aka FFU, yenye makao yake nchini Ujerumani, wameachia hewani CD mpya yenye nyimbo za 50 ya uhuru. Nyimbo zilizopo kwenye CD hiyo ni utunzi na uimbaji wake kiongozi wa bendi hiyo; Kamanda Ras Makunja...akiimba kwa kushirikiana na Chris-B, mpiga solo wa kikosi hicho. Habari za uhakika zimetonya kuwa nyimbo hizo zimetuwa pia katika Blog mashuhuri ya Michuzi, pia vituo vya Radio vya Deutch Welle mjini Bonn - Ujerumani, Radio VOA ya Washington, Radio Free Africa - Mwanza,.....vimepokea nyimbo hizo ambazo wakati wowote zinaweza kutoa burudani kwa wananchi katika shamra shamra za miaka 50 ya Uhuru. Nyimbo hizo mbili; (1). Miaka 50 Uhuru.(Rumba). na (2). 50 Uhuru shangwe. Zinasikika pia at; www.ngoma-africa.com
No comments:
Post a Comment