Wednesday, January 25, 2012

HAPA LUGHA NI GONGANA GONGANA......SIKILIZA HAPA!



Mimi huwa najiuliza sana, kwanini sisi hatuipendi lugha yetu ya Kiswahili? Maana mtu kama haongei vizuri kiingereza basi huyo anaonekana sio msomi....hata awe amesoma sana, lakini kama hajui lugha hii ya Kiingereza basi anaonekana bado. Wakati wakuongea hata kwa viongozi wetu walio wengi utasikia tu, lazima wachanganye kidogo na kimombo, la sivyo watu wanakuona shule haijapanda. Tena hata kama ukitaka kugombea uongezi wowote hasa Ubunge, kama mwenzangu na mimi hupandishi lugha hii ya Kiingereza hupati uongozi watu watasema, hajasoma huyo hata Kiingereza hajui bwana? Kumbe wewe una elimu yako nzuri tu, kasoro hujui lugha ya watu vizuri. Sasa huwa najiuliza sana kwanini tunatukuza sana lugha za watu wengine? na kusahau kuwa tuna lugha yetu nzuri tu! tena inayotumika vizuri tu! na kueleweka vizuri miongoni mwa Jamii yetu.

Hebu ona hii video ya aliyekuwa Waziri wa Ulinzi - Italy, Mh.Ignazio La Russa, akitaka kutoa pongezi kwa Serikali ya UK, lakini akibabaika kwa lugha ambayo sio yake.....hajui kabisa Kimombo, lakini pamoja na kutojua kwake Kimombo ni Waziri wa Nchi. Pia aliposhindwa kabisa kutoa shukrani hizo kwa Kimombo...aliamua kutoa salamu hizo za shukrani kwa lugha yake ya Kiitaliano. Wenzetu wanathamini sana lugha zao, wengi utasikia wanasema; Nijue Kiingeleza kwani mimi ni Mwingereza? Lakini mimi si maanishi kwamba usijue au kujifunza Kiingereza, kwani ni lugha muhimu sana Duniani, lakini pia lugha yetu tuithamini sana......sio nataka kuwa Mbunge, uwezo huo wa uongozi ninao....lakini kwasababu sijui Kimombo basi siwezi kuwa Mbunge. Mimi nashauri; mtu kama hajui kiswahili hapo kweli hastahili kuwa Kiongozi, maana atawaambia nini wananchi Watanzania wanaoongea Kiswahili.

No comments:

WATEMBELEAJI