Thursday, January 26, 2012

KICHEKESHO CHA LEO!

Mwizi mmoja, alimwona tajiri mmoja akizikwa na vitu vingi vya thamani, akasema kimoyomoyo; usiku nakuja kuliiba Jeneza lote. Giza lilipofika akaenda kuiba lile Jeneza la tajiri.....sasa amelibeba yupo njiani akakutana na Polisi wa Doria, alipowakaribia akaanza kuzungumuza kwa sauti; mimi niliwaambia wanizike Morogoro wao wamenizika Dar es salaam....sasa naenda mwenyewe Morogoro. Polisi kusikia hivyo, wote ni mbio kwenda mbele!


- Cheka basi unenepe.....kila siku kununa tu! mpaka lini?

No comments:

WATEMBELEAJI