Anaitwa Bibi Cheka, kutoka huko Bunju - Dar es salaam.....Bibi wa kizazi kipya, anarap vizuri sana, ana sauti nzuri sana....jana nilikuwa nasikiliza Radio Ebony - Iringa, kupitia mtandao alimhoji mtangazaji Eddo kwa njia ya simu, alinifurahisha sana maelezo yake....inaonekana yupo kamili sana. Pia nilisikiliza nyimbo yake mpya aliyorekodi pamoja na mwanamziki maarufu Tanzania wa kizazi kipya CHEGE, alinifurahisha sana na nimemsifu sana Bibi Cheka, anaweza sana tu!
- Haya Bibi Cheka, ukumbi ni wako.....kamata rungu, kila lakheri sana!
No comments:
Post a Comment