Haya ni maneno yaliyoandikwa katika magari ya CPPS-MISSION WATER PROJECT.......katika huduma zake Vijijini, kusaka maji na kuelimisha Jamii.
Mimi Na Peter, Tukiwa Water Project - Dodoma katika sherehe ya ufunguzi wa Shule ya Msingi ya Shirika hili la Water Project - Miyuji.
Peter...amefika leo Tanzania, tayari kuanza upya kazi mbalimbali za hapo Water Project....nami nimepata ujumbe wa kwenda huko Water Project Dodoma, na nimeitikia wito huo....sasa nipo kwenye maandalizi ya kuondoka hapa Italy moja kwa moja kurudi Dodoma nyumbani, nimekuwa nikifikiri sana kwa muda sasa, na nimepata jibu na uamzi kuwa nipo tayari sasa kurudi tena Water Project, kufanya kazi za kusaka maji na za Jamii kwa ujumla. Nimekubali kwa moyo wote na sasa nipo nafungasha vilango kuondoka, watu wengi hapa Italy wamenishauri na kuniomba nibaki....lakini uamzi wangu ni kwenda/kurudi nyumbani sasa, najua kuwa watu wengi hapa Italy watahuzunika, lakini sina jinsi. Hata mimi mwenyewe nina huzuni kidogo maana nimeishi hapa miaka 11 sasa, nimeishi na watu vizuri sana na kuwa na marafiki wengi sana, imekuwa kama nyumbani kabisa, sijawahi kupata shida na watu wala kujisikia vibaya, hivyo ni nyumbani kabisa, nitapakumbuka daima Cesena....na nipatapo nafasi nitarudi kutembelea na kuwasalimu Marafiki zangu.
Dodoma - Water Project, nimeomba sana nirudi tena kufanya kazi Vijijini, kama nipendavyo toka zamani....ila Ofisi imesema; mpaka nikifika watapanga na kuona. Nimefurahi sana kurudi Tanzania moja kwa moja, ndoto yangu imetimia ya kurudi......Naomba sana sala zenu Wadau wangu ili mambo yaende vizuri.
Kuhusu Blog hii naamini itaendelea kuwepo, kama kutakuwa na mabadiliko yoyote nitawataarifu, lakini naami nitaendelea kama hakutakuwa na mambo mengi yatakayonikabili....lakini vinginevyo nitashindwa. Mambo yakienda vizuri naamini kufikia mwezi wa nne mwishoni nitakuwa tayari Dodoma, bado sijui kwa uhakika kamili lini nitaondoka, maana mwezi wa tatu kuna mambo ya kumalizia hapa....baada ya hapo naamini nitaondoka.
- KARIBUNI SANA DODOMA, MAMBO ZAIDI NITAENDELEA KUWAJUZA!
WENU BARAKA CHIBIRITI.
No comments:
Post a Comment