Monday, February 13, 2012

MBOGA ZA MAJANI.......SWAAAAAAAAFI....!!!!!!!!


Hakika mboga za majani ndizo moja ya virutubisho bora vya afya ya Mwanadamu, binadamu huyo aitumiapo vyema mwili wake haushambuliwi na magonjwa ya mara kwa mara. Huko Vijijini mboga hizi zinapatikana kwa wingi na za kila aina. Pichani ni Watoto wa Kijiji cha Ntyuka - Dodoma, wakichuma mboga za majani ya maboga....ambayo imestawi vizuri na mazingira yake ni mazuri, si kama mboga ziliwazo Mijini hasa Jijini Dar es salaam, ambazo hulimwa katika mabonde ya maji taka.

- Picha na Mkuu Father Kidevu.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nimekumbuka nyumbani yaaani huu ndio msimu wake ww acha tu..Kule kwetu tunaiita mboga hii MBITIKU...

Rachel Siwa said...

Kaka ninasikia eti dodoma mboga ya majani ya Maboga haioshwi na ukiosha haiivi?duuhh nimeitamani sana.

Baraka Chibiriti said...

Dada Rachel, kwakweli mimi sijawahi kusikia hilo, sijui....inawezekana, si unajua tena imani za vijijini zilivyo. Watu wa vijijini wana masharti yao, wakati mwingine ukisikia unabaki kucheka tu!

Pia Dom kuna shida sana ya maji, huenda wamejipatia sababu humo humo.

@ Dada Yasinta, nimekukumbusha bombi hii nyumbi hii?

WATEMBELEAJI