Wednesday, February 29, 2012

NAFAKA ZAPAISHA KATA ZA CHAKWALE NA RUBEHO!

WAFANYABIASHARA WAKIUZA MAHINDI KATIKA SOKO LA KIBAIGWA.


Tarafa ya Gairo katika Wilaya ya Kilosa, Mkoani Morogoro.......imepata mafanikio makubwa sana hasa katika Sekta ya Kilimo, kutokana na Wananchi wake kuwa wazalishaji wakubwa wa Mahindi, Viazi vitamu, Alizeti na Ufuta. Pamoja na kilimo cha usalishaji wa mazao hayo, pia sehemu kubwa ya Wananchi wake ni wafugaji wa mifugo ya aina mbalimbali hasa ng'ombe na mbuzi.
Kutokana na mafanikio katika nyanja hiyo, Wananchi wa Tarafa hiyo hasa kutoka Kata ya Chakwale na Vijiji vya jirani pamoja na Kata ya Rubeho, wamekuwa na hamu kubwa sana ya kuendeleza mafanikio hayo kupitia Nishati ya Umeme.......lakini mpaka sasa umeme bado haujafika! Wahusika mpo hapo?....mnasikia kilio hiki?

- Habari na Mkuu John Nditi.

No comments:

WATEMBELEAJI