Monday, February 27, 2012

POLISI WAMUOKOA PADRI KANISANI..........

Padri wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Lugoba, Jimbo la Morogoro, Padri Philipo Mkunde.....amezuiwa na waumini kuongoza Misa Takatifu baada ya kudaiwa kuwakashifu Waumini wa Kabila la Wakwere. Padri Mkude, alizuiwa kuongoza misa ya hapo jana Jumapili asubuhi Parokiani hapo baada ya Waumini zaidi ya 200 kuandamana wakiwa na mabango zaidi ya 20 wakidai ahamishwe kwa kuwa amewatukana katika mahubiri yake, kwamba; watoto wao ni wachafu na wao wamebakia kucheza ngoma badala ya kufanya maendeleo.

''Tumechoka na mahubiri ya huyu Padri, kila akihubiri Kanisani lazima atuseme Wakwere, tumekosa nini??'' Mara atuseme tu maskini, mara watoto wetu ni wachafu na hatuwapeleki shule tunashindia ngoma tu....tumechoka hatumtaki kabisa (walisema Waumini maneno haya)''.

''Leo tumemzuia asisome misa kabisa, hakuna haja maana hakuna amani Kanisani hatujui ana kitu gani na sisi, sijui kwasababu Parokia hii ni Wakwere?''
Hata Jumatano ya Majivu wiki iliyopita katusema sana, eti watoto wetu ni wachafu sana ukilinganisha na Makabila mengine Tanzania, hii ni kashfa sana kwetu sisi, walisema hivi Waumini hawa wa Parokia ya Lugoba.

Wakwere ni moja ya Makabila katika Mkoa wa Pwani, linalopatikana Wilayani Bagamoyo....lakini katika mfumo wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Lugoba ipo chini ya Jimbo Katoliki la Morogoro.
Hali hiyo imesababisha watu wengi kutokwenda Kanisani wakijua leo Padri huyo anaongoza Misa, lakini akiongoza Katekista....Ibada inajaa utadhani Askofu amekuja, tunachotaka hapa ni Padri mwingine, kama Askofu anatujali atuletee Padri mwingine ''(walisema hivi Waumini hao)''.

- Habari na Gloria Tesha.

No comments:

WATEMBELEAJI