Monday, February 20, 2012

VIJANA TUJIFUNZE KWA BIDII MAISHA, TUACHENI MAMBO YA DEZO!


Ushauri kwa vijana wenzangu kuwa; tujifunze kwa bidii mambo ya maisha na kufanya kazi kwa bidii....tuacheni mambo ya dezo dezo tu! kwani dezo inaumiza.

Hatari zinazoweza kujitokeza katika ulimwengu wa sisi vijana tusipojifunza kwa bidii na kujitatafutia ufundi na uwezo wa kuchagua vipaumbele katika maisha yetu. Nawaalika vijana wenzangu kupima mambo kadiri ya uzito wake na kuyapatia nafasi yake katika vipaumbele vya maisha. Tabia ya kupenda ''dezo dezo tu'' na njia za mkato ni hatari sana kwetu sisi vijana katika maisha yetu ya siku za usoni kama Wazazi, Viongozi na Raia wema. Nawaalika vijana wenzangu kutafuta ushauri, kujichotea hekima kutoka kwa Wazee wetu na kukataa anasa na vishawishi vinavyoletwa na mafuriko ya vyombo vya habari katika ulimwengu wa Utandawazi.

No comments:

WATEMBELEAJI