Wednesday, March 14, 2012

MAMBO YA UTANDAWAZI....NA WATOTO NI SAWA?

Ni sawa mtoto mdogo aanze na mambo ya Utandawazi kwa michezo mbalimbali, badala ya kuwa mbunifu kwa kutengeneza michezo mbalimbali?

Michezo ya zamani imeanza kuishia ishia, huku kwa wenzetu ndo hamna kabisa imepotea! Nilikuwa naongea na mtu fulani wa hapa Italy.....hata wao miaka ya nyuma kulikuwa hakuna michezo mingi ya watoto hivyo walikuwa wakibuni michezo. Kwetu Tanzania ukienda Vijijini bado unaweza kuona michezo ikibuniwa na watoto, ila kwa Mijini ni shida sasa kuona michezo hiyo, maana watoto walio wengi wanataka kununuliwa michezo ya dukani, au la sivyo ni kucheza michezo ya kwenye Computer.
Je wewe Mdau unaona hii ni sawa au? Na inawasaidia watoto au?

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

kaaazi kwelikweli..natamani siku zingerudi nyuma ...

WATEMBELEAJI