Monday, March 19, 2012

TUNAMLINDAJE NA KUMSAIDIA MTOTO HUYU!

Mwanamke Mkazi wa Jijini Dar es salaam.......akiwa amembeba Mtoto mdogo ambaye haijajulikana kama ni wake au la! na ubebaji wa Mtoto huyo haupo sahihi kwani amembeba katika hali ya kuzidi kujipatia kipato licha ya jua kali kuwaka, hii ni katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi.....karibu na Kituo cha Daladala cha Msalaba Mwekundu. Mtoto huyu hajafunukwa......lakini Mwanamke huyu amejifunika kichwani kukwepa jua kali.
Mwanamke huyu akiwa katika pilika pilika zake za kutafuta ridhiki kwa njia ya kuomba omba kwa wapita njia hasa katika Magari.
Baadhi ya Wanawake na omba omba mbalimbali wamekuwa wakitumia Watoto ambao sio wao kwa shughuli hizi za kujitafutia kipato, na kushindwa kuwabeba katika njia ya usalama na kuwakinga na jua na mvua kama Mtoto huyu.

VYOMBO HUSIKA HAVINA BUDI KUCHUKUA HATUA KWA WAZAZI WA NAMNA HII.

- Picha na Mroki a.k.a Father Kidevu.

No comments:

WATEMBELEAJI