Wednesday, March 14, 2012

UMASKINI UNAVYOCHOCHEA UKATILI KWA WATOTO!

Ukatili dhidi ya Watoto ni miongoni mwa changamoto kubwa sana ambazo Jamii yetu inakabiliana nayo.
Japo kumekuwa na juhudi mbalimbali za Kisera na mafundisho kwa njia mbalimbali za kupashana habari kuhakikisha kuwa Watoto wanapata ulinzi wanaostahili, lakini bado vitendo vya unyanyasaji wa Watoto vingali vikiendelea. Wiki mbili zilizopita katika Wilaya ya Chamwino, Mkoani Dodoma.....lili ibuliwa tukio la kusikitisha la unyanyasaji wa Mtoto huyu mwenye umri wa miaka 11 ambaye alichomwa moto na Mama yake mzazi, katika kile ambacho Mzazi huyo alidai ni kumwadabisha kwa kitendo cha kuiba Sh.1,000 ambayo mwenyewe anadai aliipata kwa mbinde sana!
Shambulio hilo lililodaiwa kulengwa kumwadabisha lilimfanya mtoto huyo kujeruhiwa shingoni na usoni, baada ya kuchomwa na kijinga cha moto. Katika maelezo yake mtoto huyu anasema kuwa; aliiba fedha hiyo kutokana na njaa aliyokuwa nayo........Mama mzazi wa Mtoto huyu, Mariam au kwa jina maarufu Kijijini hapo (Manzila Sajilo) alisema kuwa; alifanya hivyo kutokana na hasira baada ya Mtoto huyo kuiba fedha hiyo ambayo alikuwa amehifadhi ndani kwa ajili ya matumizi mengine.


Wakati wa Kikao cha Bunge lililopita, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Mh.Ummy Mwalimu........aliwataka Wazazi kutoadhibu Watoto wao katika hali ya kuwafanya wawe na mfadhaiko, na yeye haamini kama kiboko au adahabu za ajabu ajabu ndio njia nzuri ya kumwelimisha Mtoto, na kutaka Wazazi wawe na tabia ya kuwakanya Watoto wao kwa kuwaelekeza sio kuwapiga.

- Habari na Sifa Lubasi, Dodoma.

No comments:

WATEMBELEAJI