Wednesday, March 14, 2012

WAKATI NYINGINE HUWA NAWAZA SANA NA KUJIULIZA MASWALI.

HUWA NAWAZA NA KUJIULIZA MASWALI.....PIA NA KUJIJIBU MWENYEWE, KWA MFANO;


1). Siku yangu nzuri kuliko zote? = Leo!

2). Kipingamizi kikubwa? = Kuogopa!

3). Kitu rahisi sana kuliko vyote? = Kukosea!

4). Kosa kubwa sana kuliko yote? = Kukata tamaa!

5). Mzizi mbaya sana wa kila kitu? = Ubinafsi!

6). Ukitaka kusahau mabaya? = Fanya kazi ni dawa nzuri sana ya kusahau!

7). Wasomi wa kubwa sana wa dunia hii? = Watoto!

8). Hitaji kubwa katika dunia hii? = Kuongea na Watu!

9). Furaha kubwa katika dunia hii? = Kuwa msaada kwa watu wanao hitaji msaada.

10). Fumbo kubwa katika dunia hii? = Ni kifo tu!

11). Mtu hatari katika dunia hii? = Ni yule mwongo!

12). Pendo baya katika dunia hii? = Kuto samehe!

13). Zawadi nzuri katika dunia hii? = Kusamehe!

14). Kuto kata tamaa katika dunia hii? = Ni maisha ya ukweli!

15). Ukarimu mkubwa katika dunia hii? = Ni tabasamu lako la ukweli kutoka moyoni!

16). Dawa nzuri katika dunia hii? = Ni Imani!

17). Nguvu kubwa katika dunia hii? = Ni Imani yako!

18). Kitu kizuri katika dunia hii? = Ni Upendo!


Haya na wewe ongeza yako hapa...........

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

kumbe tupo wengi tunaojiuliza maswali:-) Kaka Baraka umemaliza kwani umesema yote..Ahsante kwa darasa.

Anonymous said...

hongera sana kaka kazi nzuri sana na mimi naongezea nyinginekitu kbaya sana katia maisha ni kutokujiamini na kitu kizuri sana ktk hii dunia ni kufanya mambo yako kwa uwazi bila kificho na kujaribu kila kitu halimradi hufunji sheria kuna uwezekano wa kupata mafanikio udhubutu unampeleka mtu katika mafanikio na kitu kbaya sana katika dunia hiini kuwa mnafiki na kujua kuongea na kujipangilia maneno na kuongea point kutakujengea heshima nakukuwezesha kupata marafiki wengi nina mengi zaidi lakini kwa leo ni hayo tu asante kwa somo zuri kaka ubarikiwe sana

WATEMBELEAJI