Friday, March 2, 2012

WITO KWA VIJANA WENZANGU!

VIJANA TUTUMIE VYEMA FURSA ZA ELIMU ILI KUJIANDAA KULETA MABADILIKO YANAYOKUSUDIWA NDANI YA JAMII ZETU!



Tukazie kwamba; Vijana tunapaswa kuwa makini zaidi kutokana na athari za maendeleo ya Sayansi na Teknolojia katika ulimwengu huu wa Utandawazi, vinginevyo tunaweza kujikuta tukiogelea katika dimbwi la mmomonyoko wa maadili na utu wema. Ni changamoto kwetu sote vijana kujenga maisha yetu katika misingi ya sala kwa kutoa kipaumbele cha pekee cha uwepo wa Mungu katika hija ya maisha yetu ya ujana....vinginevyo ni vigumu sana kupata mafanikio tuyakusudiayo bila ya kuwa na nidhamu na maadili mema.

Vijana katika Mataifa mbalimbali wamekuwa ni chachu ya mabadiliko na mageuzi makubwa ya kijamii, kisiasa na kiuchumi, ikiwa kama tutatumia vyema fursa tunazopewa na Jamii katika masuala ya elimu na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Inasikitisha kuona kwamba; baadhi ya vijana wanachezea fursa za masomo, lakini hali kama hii inaweza kuwagharimu sana kwa siku za usoni. Mwelekeo wa sasa pasi na elimu, ujuzi na maarifa, maisha yatakuwa ni magumu kweli kweli. Hii ni changamoto kwa sisi Vijana kutumia fursa hizi kwa ajili ya kujiandaa kikamilifu ili kuleta mabadiliko yanayokusudiwa katika nyanja mbalimbali za maisha.

No comments:

WATEMBELEAJI