Saturday, November 8, 2014
AJALI; MENEJA WA NSSF NA DEREVA WAKE WAFARIKI PAPO HAPO WILAYANI MBOZI.
Gari aina ya LandCruiser, mali ya shirika la NSSF lenye namba za usajili SU 36276, Wilayani Mbozi....baada ya kugongana uso kwa uso na Lori la mafuta, jana mchana eneo la Vwawa.
Baadhi ya wanafamilia wakilia kwa majonzi makali baada ya kushuhudia ajali hiyo, iliyosababisha vifo vya ndugu zao hao wawili Dereva wa NSSF na Meneja wake.
Trecta likivuta Kibini ya Lori hilo, ili kumtoa Dereva wa Lori hilo ambaye alibanwa vibaya baada ya kutokea ajali hiyo.
Dereva wa Lori hilo akiwa amebanwa katika kibini ya Lori hilo, kabla ya kutolewa na wasamalia wema.
Baadhi ya wasamaria wema wakimsaidia Dereva aliyebanwa, wakitoa msaada baada ya kumuokoa Dereva huyo wa Lori.
- Hivi ajali hizi zitaisha lini jamani? Mbona zinazidi kutumaliza tu? Kweli hatuwezi kuzizibiti? Mbona wenzetu wa nchi za nje sio kila siku ajali......sisi kila kukicha ni ajali tu, chonde chonde jamani Wadau wenzangu hebu tuliangalie hili swala kwa umakini....maana tunazidi kuisha na hizi ajali zisizo na maana, za uzembe kila mara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







No comments:
Post a Comment