Tuesday, December 1, 2015

BUNGE KUONDOA AJIRA ZA KUDUMU SERIKALINI....KUDUMU KWA AJIRA YA MFANYAKAZI KUTATEGEMEA JUHUDI ZAKE KAZINI.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litafanya mabadiliko makubwa, sheria za utumishi wa Umma kwa kuondoa ajira za kudumu Serikalini, ili kuwezesha mabadiliko yaliyokusudiwa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Katika mabadiliko hayo, mfumo sasa wa ajira za Serikali kuwa za kudumu utabadilishwa na badala yake kudumu kwa ajira ya mfanyakazi kutategemea juhudi na bidii yake kazini, ili kuondoa uzembe uliodumu miaka nenda miaka rudi katika sekta ya Umma.
Akizungumza katika mahojiano binafsi mjini Dodoma mwishoni mwa wiki mbili zilizopita, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Job Ndugai.....alisema; baadhi ya sheria za kazi zinawafanya baadhi ya watumishi wa Umma kuwa wazembe.

No comments:

WATEMBELEAJI