Monday, December 21, 2009

FAMILIA NZIMA WAJINYONGA KUKIMBIA HALI NGUMU YA MAISHA.

Watu watatu wa Familia moja toka India yenye makazi yake katika Mji wa Dubai, wamefariki dunia baada ya kujinyonga huku mtu wa nne ambaye ndiye aliyetoa wazo hilo la kujinyonga amenusurika maisha yake.
Kwa mujibu wa gazeti la Gulf News, baba mmoja wa kihindi aliwashauri wanae na mkewe wajinyonge kwa wakati mmoja ili kukimbia hali ngumu ya maisha iliyokuwa ikiwakabili. Siku ya jumatano iliyopita mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 40, mkewe mwenye miaka 38, watoto wao; wakiume mwenye miaka 22 na mtoto wa kike mwenye miaka 20, walijifunga kitanzi na kujitundika kwenye Feni la kwenye Dari la nyumba yao iliyopo kwenye maeneo ya Karama mjini Dubai, ili wafariki wote kwa wakati mmoja.
Baba wa Familia hiyo alikiri kuwa yeye ndiye aliyetoa wazo la kujiua, alisema mkurugenzi wa kitengo cha makosa ya jinai cha Dubai, Bw.Khalil Ebrahim alipokuwa akiongea na gazeti hilo.
Baba huyo aliwaambia Polisi kuwa kitanzi chake kilichoropoka toka kwenye Feni na hivyo kunusurika maisha yake, wakati mkewe na watoto wake hawakuwa na bahati kama yake, na wote walifariki dunia kasoro yeye Baba. Familia hiyo iliacha barua ikisema kuwa hali ngumu ya kiuchumi ndiyo iliyofanya wachukue uamzi huo.
Mwanaume huyo alikuwa akimiliki duka la nguo lililopo kwenye ghorofa alilokuwa akiishi na familia yake. Biashara yake ilikuwa haimuendei vizuri kama kawaida siku zote.
Dubai inakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi na madeni makubwa kufuatia mtikisiko wa mfumo wa fedha duniani.
Ni habari ya kusikitisha sana.

No comments:

WATEMBELEAJI