Hapa Berlusco akijaribu kuinuka ili amwangalia, amtambue aliyemtupilia sanamu ambayo ilimwumiza.
Jamaa mwenyewe aliye mpiga Waziri Mkuu Silvio Berlusconi, huyu hapa anaitwa Massimo Tartaglia miaka 42. Sasa kesi anayo kubwa, ingawa watu wengi hapa Italy wanamtetea na kusema hana akili sawasawa kutokana alishawahi kupata matatizo ya akili toka utotoni mwake. Na wengine kusema kwamba alitumwa na chama pinzani kutokana kumekuwa na mzozo mkubwa sana wakati huu na chama pinzani, na wengi kumchukia waziri mkuu huyu. Ila jamaa aliye mpiga baada ya kuhojiwa amedai yeye hajatumwa na mtu yoyote wala kuwa upande wa kundi la chama chochote isipokuwa hampendi kabisa hata kumsikia Waziri Berlusconi kwa mda mrefu. Hapa kazi ipo kweli kweli!
No comments:
Post a Comment