Hospital ya Meldola nchini Italy, karibu na hapa ninapo ishi, yapata uamzi wa kuungana na Hospital ya Bugando ya Jiji la Mwanza - Tanzania, kwa kupigana kikamilifu na gonjwa la kansa. Madaktari wa Hospital hiyo ya Meldola wameamua kuchukua uamzi huo ili kusaidia wagonjwa mbalimbali huko Mwanza na Tanzania kwa ujumla wenye matatizo mbalimbali ya magonjwa ya kansa. Nasi watanzania tunawashukuruni sana kwa uamzi wenu huo mzuri wa kusaidi katika tatizo hilo la kansa.
No comments:
Post a Comment