Friday, February 26, 2010

WANAWAKE WA KIMASAI KUWAPELEKA WATOTO WAO SHULE.

Wanawake wa jamii ya wafugaji kutoka kabila la kimasai katika kijiji cha Wami Sokoine, Wilaya ya Mvomero, Mkoani Morogoro, wameazimia na kuhakikisha kuwa watoto wao wote wakiume na wakike wanapata elimu ipasavyo kuanzia awali hadi kufikia vyuo vikuu, ili baadae waweze kukabiliana na mabadiliko ya Dunia ya Utandawazi.
Hayo yameelezwa na wanawake wa jamii hiyo ya kimasai kwa nyakati tofauti baada ya kumalizika kwa maafali ya 39 ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari ya Lutheran Junior Seminary ya Morogoro, yaliyofanyika shuleni hapo.
Katika maafali hayo kijana pekee wa jamii ya kimasai Ninoo Palanda, alikua ni miongoni mwa wahitimu 97 waliofanya mtihani wa Taifa wa kidato cha sita na kushiriki kwenye maafali hayo.

Pichani: Mhitimu wa masomo ya kidato cha sita Ninoo Palanda akiwa pamoja na mama yake na baadhi ya wanandugu kutoka Wami Sokoine, wakati wa sherehe hiyo iliyofanyika shuleni hapo Februari 21 mjini Morogoro.

-Hongera kwa akina mama hao wa kimasai wa Wami Sokoine, kwa kufikia uamzi huo wa kupeleka watoto wao shule, kwani shule ni mhimu sana katika haya maisha na wala si kuchunga ng'ombe tu.

No comments:

WATEMBELEAJI