Thursday, March 18, 2010

JE VITUO VYA KUPUMZIKIA ABIRIA KWENYE VITUO VYA DALADALA NI HAKI AU HISANI?

Ndugu Baraka;

Naomba uweke kilio hiki kwenye globu yako ili wadau na madhamana wachangie.
Wakati wa shirika kongwe la usafiri Dar es salaam (UDA) vituo vya kupumzikia abiria vilijengwa kwenye ruti zote za jiji kukiwa na alama za kuonyesha kuwa ni kituo cha basi na ratiba za mabasi ziliwekwa na kuzingatiwa, na kila abiria alifika kituoni kwa wakati wake kulingana na umuhimu wa safari zake.

Mambo haya sasa ni historia kwa mfumo wa mabasi ya daladala ambayo hayana ratiba maalum na maandamano kwao ndiyo kazi - maisha na vituo vya kupumzikia abiria havipo wala si muhimu kwa abiria.

Utaratibu huu wa usafiri usio na ratiba maalum na huduma bora kwa abiria unaliweka Jiji la Dar es salaam nje ya orodha ya majiji ya kimataifa na kufanya wageni kubaki na mshangao wanapotembelea Tanzania na kushindwa kufanya utalii Jijini.

Je wadau hiyo hali itaendelea hadi lini kwa abiria kuungua jua na kunyeshewa mvua ndani ya Jiji lao?

Mdau wa usafiri wa daladala
Dar es salaam.



-Ni kweli kabisa Mdau umeongea jambo zuri sana, maana Jiji letu hakuna utaratibu wa usafiri ni fujo tu kila kukicha kwanini? Pia hawa wa daladala sio tu hawana mpangilio wa usafiri bali fujo za kuendesha vibaya, kugongana kila mara na kuhatarisha maisha ya abiria, jambo hili ni kero sana kwanini lisishughulikiwe ipasavyo? Mkuu wa mkoa, Meya wa Jiji, wakuu wa Wilaya na viongozi mbalimbali wa Jiji Kazi kwenu kwa jambo hili kulikazia umuhimu!
Asante sana mdau wa usafiri wa daladala Dar.

No comments:

WATEMBELEAJI