Thursday, March 11, 2010

JOHAN LORBEER MJERUMANI ANAEGANDA UKUTANI.






















Cheki maajabu haya, jamaa Johan Lorbeer wa huko nchini Ujerumani, akionyesha ujuzi wake wa kuganda ukutani, na watu wanashangaa sana haya maajabu, anawezaje kuganda ukutani bila kushikiria?, hakuna waya wala kitu chochote kinacho mshikiria (unachoweza kukiona)....ila kutakuwa kuna mbinu fulani imetumika, sasa sijui ndo mazingaombwe yenyewe haya?






1 comment:

Simon Kitururu said...

Anachofanya sio mazingaombwe. Waliodai kumuona akijiandaa kuning'inia ukutani KWA MKONO wanadai kuwa mkono ugusao UKUTA huwa ni feki ambao unakuwa umeshikizwa ukutani na sukurubu na ndio hutengenezwa kumsapoti mwili mzima . Na anachofanya KWA USTADI ZAIDI ni kuficha mkono wake wa kikweli na watu kufikiri kaning'inia kikweli kwa kugusa tu ukuta. Na nafikiri hata agangapo kwa miguu hutumia aina za triki zisizocheza mbali na hivyo.

Atleast hiyo ndio waliomshuhudia akiandaa onyesho hudai huwa anafanya ndio maana huwa hagandi katika jengo lolote tu umchagulialo ambalo hajaliandaa.

WATEMBELEAJI