Mwasisi wa Habari za Jamii mtandaoni (Social media) nchini, Bw.Muhidin Issa Michuzi (pichani) safarini kuelekea London - Uingereza, kuhudhuria kongamano la pili la watanzania waishio nchi za nje (Diaspora 2 conference) kwa mwaliko maalumu akiwa kama blogger.
Bw.Michuzi, ambaye ametoa mchango mkubwa sana katika kupromoti habari za Jamii mtandaoni kupitia blog yake maarufu sana ndani na nje ya nchi iitwayo; issamichuzi.blogspot.com. Amealikwa huko mkutanoni na ubalozi wetu Uingereza ili kutoa mada inayohusu umuhimu wa habari za Jamii mtandaoni katika kujenga daraja kwa walio ndani na nje ya nchi.
-Tunakutakia kila lakheri nyingi sana huko Uingereza katika kikao hicho, Mzee wa libeneke, Ankal, Mdau namba 1.
1 comment:
Tunamtakia safari njema sana na arejee nyumbani salama kwa ajili kutuhabarisha wadu wake.
Post a Comment