Tuesday, March 23, 2010

JE SOKA LA TANZANIA LINAWEZA KUCHANGIA CHOCHOTE KATIKA PATO LA TAIFA?

Kila mwaka wanazuoni wa wizara ya fedha na mipango nchini Tanzania wanatengeneza bajeti ya mapato na matumizi ya Serikali kwa kuzingatia vyanzo vikuu vya mapato visivyopo na kuibua vipya.

Wakati hayo yakiendelea sina uhakika sana iwapo wanazuoni hao wamenusa na kuona iwapo soka la Tanzania linaweza kuwa miongoni mwa vyanzo vikuu vya mapato kama ilivyo kwa sigara na bia.

Ni kweli kuwa lile soka la enzi za ujima halikuonyesha mwelekeo mzuri wa kuweza kutoa mchango ufaao kwa makusanyo ya ushuru na kodi, lakini hili soka la teknohama lina nafasi nzuri ya kutoa mchango huo iwapo sasa Serikali itakuja na sera madhubuti ya kubadili mfumo wa usajili wa wachezaji na klabu za soka. Taifa linahitaji kuwa na klabu za soka zilizo mahiri na makini katika tasnia ya utawala na fedha ili jamii inufaike kiuchumi na siyo kuishi kwenye mdumange na mdundiko kila msimu wa ligi kuu unapomalizika.

Wasalaam na shukrani;

Ray Ephraim Ndewingiya Njau
Mdau wa utamaduni na michezo
Dar es salaam - Tanzania.

No comments:

WATEMBELEAJI