Monday, May 10, 2010

KATIKA KUIPA NGUVU TIMU YETU YA MJI WA HAPA CESENA!


Rafiki Cappo, akifurahia ushindi katika kipindi cha kwanza kuisha, Cesena ikiwa inaongoza kwa bao moja bila, akiwa na gazeti lenye picha ya mchezaji wa Cesena (MALONGA) Mwafrika kutoka Kongo.





Cappo akifurahi na bia kabla ya kuingia uwanjani kwa kushuhudia mechi.


Na mimi nikifurahi na mashabiki wenzangu wa timu yetu ya Cesena, kwenye kona ya mashabiki, hata unilipie tiketi ya VIP siendi nyoo...!!!!, huku kwa mashabiki nafurahi sana. Mzee mmoja huwa anang'ang'ania tuende nae sehemu ya VIP, amejaribu mpaka ameshindwa mwenyewe. Hapa hunitoi hata kidogo.




Inaitwa CURVA MARE = Kona ya bahari ya mashabiki, hapa ndipo nilipo mimi.
Juzi niliamua kwenda kupoteza mawazo kidogo na kupumzisha kichwa, kwa kufurahia mchezo wa mpira kati ya Cesena - Padova, ambapo tulifurahi sana baada ya ushindi wa Cesena kwa mabao 2 bila, sasa tunaota kuchezea Daraja la kwanza la Italia ( Serie A) maana bado michezo miwili ili iishe ligi, nasi ni wapili kwasasa kwenye Daraja la pili...tunamategemeo makubwa. Tulifurahi sana mimi na rafiki yangu Cappo kwa ushindi huo, Cappo ni rafiki wa kweli kwangu toka nimefika hapa Cesena. Na tu mashabiki wakubwa wa Cesena.




No comments:

WATEMBELEAJI