Monday, May 10, 2010

RAFIKI ZANGU WA OVERLAND NDANI YA AFRIKA.

















Nawapenda sana jamaa hawa wa OVERLAND - ITALIA, na malori yao ya njano, katika kusafiri kwao sehemu mbalimbali Duniani, kuelimisha jamii na kusaidia kwa misaada mbalimbali, hasa Barani kwetu Afrika.
Pia wananikumbusha mbali sana, wakati nikihangaika na magari madogo, pia malori kama wao, katika kusaidia watu huko Vijijini kwetu Tanzania katika huduma ya Maji safi, wakati huo nikiwa na; CPPS MISSION WATER PROJECT, tulihangaika sana usiku na mchana, kukwama, kulala porini, kuumwa na mbu n.k. Lakini pamoja na shida zote hizo nilikuwa napenda sana kazi hiyo hata sasa bado napenda sana. Pia wananigusa sana hawa jamaa wa Overland nikiona Lori zao aina ya IVECO MAGIRUS DEUTZ, ambazo hata mimi nilikuwa mara moja moja nikiendesha, wakati huo damu inachemka kweli kweli... siambiwi kitu wala siogopi kitu...popote napita na hiyo Lori mpaka basi.
-HONGERENI SANA OVERLAND KWA MAMBO MNAYO YAFANYA, NA POLENI SANA KWA SHIDA MNAZO ZIPATA KATIKA SAFARI ZENU DUNIANI, MIMI NAWAELEWENI VIZURI SANA BAADA YA MIMI PIA KUPITIA HUMO.




No comments:

WATEMBELEAJI