Tuesday, May 4, 2010

MAZISHI YA WATOTO WALIO UWAWA NA MAMA YAO.





Mtaa wa Kariwa, Kata ya Rau, Manispaa ya Moshi, uligubikwa na majonzi makubwa sana, wakati watu walioshiriki maziko ya watoto watatu waliouawa kikatili na Mama yao mzazi.
Mama huyo kwasasa yupo Hospitalini KCMC akipatiwa matibabu ya akili. Maziko hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali na wanasiasa wengi.
Mama mzazi wa watoto hao, kwa jina Benedicta Thadei (44), mnamo Aprili 29 majira ya saa 12:oo asubuhi aliwaua watoto wake hao kwa kuwakata kata na shoka, watoto Antony Thadei (3), Noela Thadei (5) na Rose Thadei (13) ambaye pia alikuwa na ulemavu wa akili na viungo.
Mtuhumiwa huyo pia alimjeruhi vibaya mtoto mwingine Pascal Thadei (9) ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa matibabu.
Pichani ni Baba wa marehemu ya watoto hao, Aloyce Thadei ( mwenye tai na shati jeusi) akiinama kwa uchungu na kulia kwa uchungu sana mbele ya majeneza ya watoto wake wapendwa.

No comments:

WATEMBELEAJI