URAIA NA HAKI YA KUSHIRIKI MCHAKATO WA UCHAGUZI MKUU TANZANIA KWA MWAKA HUU WA 2010.
Wananchi wengi wamechoshwa na siasa za chuki, uhasama na kulipizana kisasi, changamoto kwa wanasiasa kuhakikisha kwamba wanatekeleza wajibu wao kikamilifu kwa kuhakikisha wanashiriki katika kuchangia dhamana ya kudumisha Amani, Usalama na Utulivu kati ya watu.
Viongozi watakao chaguliwa ni kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya wananchi wa Tanzania, bali si kwa manufaa yao tu wenyewe. Ili kusonga mbele katika harakati za kujikwamua kutoka katika ujinga, umaskini na maradhi, na hatimaye kujipatia maendeleo endelevu, wananchi kwa ujumla wanapaswa kuwa makini katika zoezi hili zima la uchaguzi huu ujao.
Wahakikishe kwamba wanachagua watu wenye maadili mema na wenye sifa za kuongoza. Vijana wasiwe ni washabiki tu wa vyama vya siasa bali wanatakiwa kushiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa shughuli za upigaji kura, na watambue nini wanakifanya sio kushabikia tu na hapo baadae kuchagaua viongozi wasio tufaa.
No comments:
Post a Comment