Wednesday, June 16, 2010

E-MAIL YA MALALAMIKO KUTOKA KWA RAFIKI YANGU VALENTINA.


Valentina akiwaiga nguruwe huko Makalala - Mafinga - Iringa.


Valentina akifurahi na noti za Tz, wakati alipo wasili Jijini Dar es salaam.

Valentina na rafiki yake Laura, wakisaidia kwa kazi ya kupukuchua mahindi ya watoto yatima wa Makalala.
Leo nimeandikiwa barua pepe na rafiki yangu Valentina, ambaye akionekana kwenye picha hapo juu, ana lalamika kwamba kwanini si tafsiri habari kwa kiitaliano? Anasema yeye ni mpenzi wa blog hii, huwa anapitia pitia kuangalia hasa picha za Tanzania, maana yeye na TZ haambiwi kitu, siku alipokuwa akirudi Italy ilibidi tufanye kazi haswa ya kubembeleza, ili akubali upanda ndege kurudi kwao. Sasa anasema kwanini nisitafsiri ili faidike zaidi? Marafiki zangu wa hapa wamekuwa wakinilalamikia sana kuhusu swala hili, ila mimi kwakweli sina mda sana wa kuandika lugha mbili, maana inabidi nifikiri sana; na kutafsiri si mchezo, yeye anasema hivyo hivyo tu! wataelewa. Mimi nashindwa pia nafasi inakuwa ndogo sana, ukizingatia hii si kazi kamili bali ni hobi tuu. Sasa walau nitakuwa nawalidhisha kwa maneno machache mara moja moja, pia kwa video mbalimbali hasa za miziki ya kwao nitakuwa nawawekea, au sio wadau wangu? Vinginevyo kichwa kitakosa nywele kabisa kwa kukikuna. Napenda kumjibu hapa hapa ili aone umuhimu na kwamba tunamjali!
-Carissima Valentina, ho ricevuto la tua Mail per la tua richiesta, per tradure in Italiano questa pagina di questo blog. Purtroppo non ci riesco a sodisfare il tuo desiderio, perchè sono molto impegnato di tante cose, se ci metto anche a scrivere due lingue sono finito. Mi dispiace tantissimo, comunque appena ho tempo scriverò anche in Italiano ogni tanto. Poi da oggi ogni tanto metterò qualche video divertente in Italiano, questo si che ci riesco.
Tante belle cose, un abbraccio forte. Baraka.



3 comments:

ray njau said...

POLE SANA NA HONGERA SANA.JITAHADA ZAKO BINAFSI ZA KUISADIA JAMII YETU ZINATHAMINIWA SANA.

Baraka Chibiriti said...

Asante sana Mkuu Ray.

Nasi hatuna budi kujitahidi zaidi na zaidi katika maswala haya.

ray njau said...

Umesema kweli kaka Baraka.
Kutoa ni moyo na siyo utajiri,tafadhali sana usichoke kuendelea kuwasaidia wenye uhitaji.

WATEMBELEAJI