Thursday, June 24, 2010

NILIONGEA NA WATOTO NIWAFUNDISHAO WIMBO WA KISWAHILI.

Leo nilipata nafasi ya kuongea na watoto niwafundishao wimbo wa kiswahili, maana tumefikia karibu na mwisho sasa, na tukaona tupumzike kidogo ili waniulize maswali kidogo na kutaka kujua Tanzania na Afrika kwa ujumla. Mara nyingi watu huniuliza maswali mengi na yaajabu sana, mara ya kwanza nilipofika tu hapa Italy, siku za kwanza kwanza nilikuwa nikikasirika sana kwa maswali ya ajabu ajabu, lakini baadae nilikuja kugundua si kosa lao kabisa, kutokana na televisheni, magazeti na vyombo vya habari kwa ujumla, mara nyingi wanaongelea buga za wanyama tu, au kuonyesha sehemu maskini za pori tu! Sasa wengi hufikiri sisi tunaishi maporini tu! Kwakweli wale ambao hawajatoka kabisa nje ya nchi yao, ukimwambia hata nyumbani kwetu nalala kwenye kitanda hawezi kukubali kabisa, wanasema Afrika yote ni ya vijumba vya majani. Sasa rafiki yangu Isabella, ambaye ni mwalimu wa hawa watoto aliniomba niongee nao na kuwaelimisha kidogo kuhusu Afrika, basi maswali yalianza ya wanafunzi hawa kama kawaida maswali mengi na yaajabu ajabu, ila moja lilinichekesha sana na sikutegemea kabisa, mototo mmoja aliniuliza hivi;

Eti nimeambiwa na Babu yangu kuwa nyinyi waafrika huwa hamfanyi kazi ndo maana maskini, hampendi kabisa kufanya kazi....huwa mnakaa tu chini ya miti ya minazi, mkisubiri nazi zidondoke. Ni kweli???
Darasa zima kicheko...hata mimi ilibidi nicheke kwa sana, sikutegemea kabisa swali kama hili, je nyinyi wadau hapa, mtajibuje swali hili?

1 comment:

mangi said...

Na mimi nacheka kisawasawa kwa kuwa siyo kosa lake bali kosa la teknolojia na habari kuisahau Afika.

WATEMBELEAJI