Thursday, July 8, 2010

AJALI YA PIKIPIKI GAZETINI HISTORIA KAMILI YA KIJANA MARKO!

Kijana Marko Venturi, ambaye alikuwa akijiandaa kwenda Tanzania hivi karibuni, na mara nyingi ameenda huko Tanzania, bahati mbaya mauti yamemkuta kabla ya safari yake, ambapo alipata ajali mbaya ya pikipiki na kupoteza uhai wake. Risala ya maisha yake ilisomwa kanisani jana katika misa ya mazishi yake, na aliyeisoma ni mtoto wake Luka wa miaka 10, kanisa zima liliangusha vilio kwa majonzi makubwa, hasa kwa maneo aliyo kuwa akiyatamka mtoto wake huyo katika kusoma risala hiyo, alisema; Baba yake Marko alikuwa akipenda sana Afrika - Tanzania, na alikuwa akimwahidi vitu vingi katika maisha karibu vyote alitimiza bila kuwa mwongo, mara ya mwisho aliahidi kuwa atajenga kituo cha watoto yatima na shule ya ufundi mbalimbali huko Dar es salaam - Tanzania ili kusaidia jamii ya Tanzania. Sasa Baba uliahidi kuwa utajenga shule na kwasababu wewe ulikuwa ni mtu wa ahadi ulitimiza daima kila ahadi zako, nasi huku tuliobaki tutakutimizia ahadi yako hiyo ya kujenga shule na kuipa jina lako kwa heshima zote. Kwa kawaida mila na desturi za hapa Italy mtu akiaga dunia mazishi yake hupambwa kwa maua ya ghalama, lakini hapo jana walitangaza kuwa watu wasinunue maua kwa mazishi hayo, bali hela hizo zitumike kuanza ujenzi wa shule ambayo marehemu Marko ilikuwa ndio ndoto yake, ili hiyo ndoto iweze kutimizwa. Kwakweli mtoto Luka, aliliza wengi sana hata mimi mwenyewe majonzi yalinitoka bila kujizuia, maana aliisoma kwa makini hiyo historia ya baba yake mpendwa na kusisitiza mambo mengi hasa la ujenzi huo wa Tanzania. Pia kwenye gazeti la mji huu leo imetoka historia yake na picha yake Marco, ndogo upande wa kulia mwa gazeti na picha kubwa ni kanisani wakati wa mazishi hayo.

Gazeti hili linasema kwa kifupi tu hasa kichwa cha habari ni kuwa;

IL MIO PAPA' MANTENEVA SEMPRE LE PROMESSE, SULL'ALTARE LETTO UN TEMA DEL FIGLIOLETTO LUCA, 10 ANNI.

=BABA YANGU ALIKUWA AKITIMIZA AHADI DAIMA, MBELE KWENYE ALTARE ALISOMA RISALA MTOTO WAKE LUKA, MWENYE MIAKA 10.

-Mungu akulaze pema peponi Marco, nasi tutakukumbuka kwa mema mengi uliyo yafanya hasa katika Tanzania yako, kama ulivyokuwa ukisema wewe katika usemi wako mara nyingi - Tanzania yangu.

No comments:

WATEMBELEAJI