Thursday, July 8, 2010

AJALI YA PIKIPIKI ILIVYO MKATISHA MAISHA KIJANA MMOJA!

Leo nilikuwa kwenye mazishi ya kijana mmoja wa kitongoji cha Ronta karibu na hapa Cesena. Kijana huyo alikuwa na umri wa miaka 38 amefariki kwa ajali ya pikipiki, ameacha mke na mtoto mmoja. Nilipigiwa simu na Padri mmoja ambae ananifahamu kwa umbali, kuwa nihudhurie mazishi hayo kwasababu kijana huyo alikuwa anajiandaa kwenda Tanzania mwishoni mwa mwezi huu kwenye misheni fulani kwaajili ya kusaidia mambo mbalimbali ya kijamii hasa ya watoto, basi bahati mbaya mauti yamemkuta katika ajali iliyo usisha pikipiki yake na wengine, jumla watu watatu wamepoteza maisha yao katika ajali hiyo. Sasa familia yake wameamua kuchangia hela kujenga kitu fulani huko Tanzania kama kumbukumbu yake, maana alikuwa anapenda sana mambo ya Tanzania.

-Mungu aipumzishe roho ya marehemu huyu mahali pema peponi, amina!

No comments:

WATEMBELEAJI