Saturday, October 9, 2010

BIASHARA YA NYANYA KATIKA BARARARA YA MIKUMI TO IRINGA.

Mimi hupita barabara hii mara nyingi sana, Mikumi to Iringa. Maana huwa naelekea huko Mafinga - Makalala katika kituo cha watoto yatima. Mara nyingi huwa nasimama kuongea na hawa akina mama wauza nyanya, lawama zao nyingi huwa; hawana soko kabisa kwa kuuza nyanya zao. Hivi kweli Taifa kama letu hili la Tanzania hatuwezi kuimarisha biashara kama hizi kwa kutafuta masoko mazuri kabisa ya bidhaa kama hizi? Mbona ni utajili mkubwa wa kuweza kuwaweka watu katika hali nzuri kabisa ya kimaisha? Watu wanamoyo sana wa kujituma katika mashamba yao na kupata mazao kama haya kwa wingi sana, baadae kazi zao zinakuwa hazina maana kabisa, maana hawapati soko kabisa. Huwa najiuliza sana, hivi viongozi wetu huwa hawaoni haya au hawapiti kabisa katika barabara kama hizi??? Mbona huwa nakutana na mashangingi (Magari) ya serikali mengi tu katika barabara hiyo. Basi sipendi kulaumu daima viongozi wetu, lakini huwa inaniuma sana kuona bidhaa kama hizi nyingi tu za kutosha hazina soko kabisa, wakati sehemu nyingine za Tanzania hakuna bidhaa kama hizi kabisa na ni shida sana kupata, ambapo wangepelekewa wangenunua na kukuza soko zaidi ya bidhaa hizi. Pia nasikitika sana kwa hawa akina mama kwa bidii zao za kulima ili wajipatie maisha bora, lakini hawawezeshwi kwa mambo madogo tu ambayo yanawezekana sana.
AKINA MAMA HONGERENI KWA BIDII ZENU ZA KAZI. IPO SIKU MUNGU ATAWASIKIA KILIO CHENU TU!

No comments:

WATEMBELEAJI