Wednesday, October 27, 2010

JAMAA MWENYE VISA NA UBAGUZI NA WAGENI HUKO SWEDEN!

Nilikuwa nasoma sasahivi gazeti moja la hapa, kuhusu huyo jamaa kwenye njama na ubaguzi mkubwa sana na wageni wote huko Nchini Sweden, ambaye anaua wageni kwa kuwashuti, na mpaka sasa amefikisha watu 50 aliye waua. Hali hii inatisha sana na kuhuzunisha sana, kuona bado Duniani kuna ubaguzi wa namna hii wa hatari sana. Baada ya kusoma habari hii nimesikitika sana, na kuwaomba ndugu zangu Watanzania waishio huko Sweden muwe makini na hatari hii, maana habari inasema mara nyingi anashuti usiku. Kwahiyo msitembee usiku kwasasa na muwe makini sana. Polisi wanaumiza kichwa kumpata huyu jamaa lakini bado ni ngumu kumpata kwake.

-TUNAKUOMBA SANA MWENYEZI MUNGU BABA YETU UTUSAIDIE KWA JAMBO HILI, WASIENDELEE KUFA WATU WASIO NA HATIA YOYOTE, AMBAO WAPO HUKO NCHINI SWEDEN KATIKA KUTAFUTA MAISHA NA KWA SABABU MBALIMBALI ZA KIMAISHA, MUNGU TUSAIDIE!

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Kaka baraka asante sana kwa maombi yako na mzidi kutuombea: Pamoja daima.

WATEMBELEAJI