Sunday, October 31, 2010

JUMAPILI NJEMA NA UCHAGUZI MWEMA SANA TANZANIA!

Ee Mungu Mwenyezi Baba wa milele, ndiwe unayeongoza mambo yote Mbinguni na Duniani, usikilize kwa wema wako Dua zetu sisi Taifa lako la Tanzania...katika swala hili la uchaguzi ambalo tunalo leo hii. Tunakuomba Amani maishani mwetu na utupatie viongozi wema wanao faa kutetea wanyonge na kuangalia zaidi maslahi ya wananchi, si maslahi yao binafsi.
Tunakuomba sana Baba utujalie Amani yako maishani mwetu!

TAFAKARI YA JUMAPILI HII; NA KUMWOMBA MUNGU NEEMA YAKE MAISHANI;

Ee Mungu Baba nimekuita kwa maana utaitika, utege sikio lako usikilize neno langu.
Ee Mungu Baba unilinde kama mboni ya jicho, unifiche chini ya uvuli wa mbawa zako.
Ee Mungu Baba Mwenyezi wa milele, utuwezeshe kufuata daima mapenzi yako Matakatifu na kuitumikia fahari yako kwa moyo mnyofu.
Amina!

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Mungu wabariki watanzania waweza kufunguka na kuchagua kiongozi mwema.

WATEMBELEAJI