Kitu gani kinitenge nawe Mungu wangu, kitu gani kinitoe kwako. Je ni dhiki? sikuja na kitu chochote Duniani, Je ni uchi? Je ni njaa? wengine wanakufa nayo, hakuna cha kunitenga nawe! Nishike mkono Ee Mungu wangu, nishike mkono nakukimbilia, usiniache peke yangu kwani wewe ndiwe kimbilio langu, kwasababu shetani ananiwinda kila siku anataka kuniangamiza. Nikupendeze wewe tu Mungu wangu.
Kitu gani kitanitenga nawe Baba yangu! Je ni mwili huu nilio nao utanitenga nawe, utanitoa nawe, mbona ni udongo tu! hauna thamani yoyote, mimi ni mavumbi tu! na mavumbini nitarudi tu! Hata nikivaa vizuri vitu vya thamani, bado ni mavumbi tu! kifo kinaningojea. Hata uhai huu nilio nao umenipa wewe Bwana tena bure hakuna ghalama yoyote. Ukiamua nife leo hakuna wa kupinga, hata mpenzi wangu, rafiki zangu, wazazi wangu n.k hawawezi kupinga, je ni nini basi kinitenge nawe....mbona sababu sina ya kunitoa kwako, je ni ndege, treni, gari, baiskeli na vitu mbalimbali vya kidunia vitanitenga nawe? Hakuna hakuna hakuna kabisa! mbona vitu vyote umenipa wewe, mamlaka niliyo nayo ni yakupita tu! nisaidie Ee Mungu wangu nisimame nawe siku zote za maisha yangu.
WEWE NDIWE KIMBILIO LANGU DAIMA SIKU ZOTE!
No comments:
Post a Comment