Saturday, October 23, 2010

WEEKEND NJEMA NA JUMAPILI NJEMA SANA KWENU NYOTE!

NINAKUPENDA SANA EE MUNGU WANGU!

Ee Baba yangu, Mungu wangu mimi nakupenda sana, umeniokoa, umenisamehe dhambi zangu. Nikitazama Dunia jinsi ulivyo iumba, nikitazama Milima jinsi ulivyoiumba, nikitazama Bahari jinsi ulivyo iweka, Wanyama maporini, samaki baharini na ndege angani, umenipa nivitawale kweli Mungu wewe ni mwema sana kwangu. Tangu uumbaji Bwana kanifikiria mema mengi, pale aliponiumba kwa mfano wake yeye nimwelezeje Mungu wangu enyi Mataifa mnisikie? Ni mwelezeje Bwana Mungu wangu...kweli nakushukuru sana. Hakuna aliye kama wewe Baba, hakuna mwingine kama wewe Baba, hakuna wa kulingana nawe Baba.

Sifa za Bwana zivume, Mungu wewe ni mwema sana, Bwana kama si wewe mimi ningekuwa wapi? kama si wewe Mungu mimi ningeitwa nani? Tazama umenitoa mbali, umeniinua machoni pa mataifa, umeniketisha chini pamoja na wakuu. Nikurudishie nini kwa wingi wa fadhili zako, Utukufu, Heshima, vyote ni kwako Bwana Mungu wangu.

ASANTE SANA BABA MUNGU WANGU MPENDWA SANA WA MOYO WANGU!

No comments:

WATEMBELEAJI