Thursday, October 14, 2010

SALA ZANGU KATIKA KUMKUMBUKA MWALIMU NYERERE.

SIKU YA LEO NAKUKUMBUKA KWA SALA ZANGU BABA.


KABURI LA BABA WA TAIFA, MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE.






BARUA NA SALAMU NYINGI SANA KWA BABA WA TAIFA, MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE;
-Kwako mpendwa sana wa Taifa letu la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Ni miaka kumi na moja sasa imepita tangu kutokea kifo chako Baba, haupo nasi ki mwili lakini tunakukumbuka daima, upo nasi mioyoni mwetu daima sisi wanao wa Taifa lako la Tanzania.
Mpendwa sana Baba wa Taifa! ni ukweli ulio wazi kuwa wewe Baba yetu mpendwa jina lako lina historia ndefu sana na ambalo halitaweza kufutika mioyoni mwetu na kwenye vitabu vinavyoeleza chimbuko la Uhuru wa Tanzania na Amani tuliyo nayo.
Mpendwa sana Baba wa Taifa! ni imani yetu kuwa kwa mapenzi ya Mweyezi Mungu kwa miaka hii kumi na moja, huko uliko utakuwa umetumiss sana sisi wanao wa Tanzania, hata sisi ni hivyo hivyo tumekumiss sana tena sanaaa....!!!! wanao tuishio tukijivunia Utanzania wetu kwa misingi uliyo tujengea na waasisi wenzako tangu enzi za kutafuta Uhuru na hatimaye mkaupata Uhuru huo toka kwa wakoloni, ambapo Amani na Utulivu vimeendelea kutawala hadi sasa nchini kwetu.
Mpendwa sana Baba wa Taifa! ushirikiano wako na mwenzio aliyekuwa Rais wa Zanzibar, hayati Abeid Amani Karume ni lulu inayo lifanya Taifa letu liendelee kustawi na kujipatia heshima Duniani kote. Jitihada zako na mwenzio zinatupa nafasi ya kujitanua na kuinjoi Utaifa wetu popote pale. Ila kuna watu wachache tu! ambao wanazidi kuubeza Muungano wakitoa sababu kede kede, lakini hawajafanikiwa kuuvunja Muungano huu, na hilo tunajivunia mpaka sasa na tunawaombeni sana wewe na mwenzio huko mlipo mzidi kutuombea ili tudumu daima na Muungano huu kwani sisi sote ni ndugu moja katika Muungano huu. Udumu Muungano daimaaa...!!!!
Mpendwa sana Baba wa Taifa! katika miaka hii kumi na moja tangu Mola akutangulize huko kwenye makao ya kudumu, Tanzania yetu hii inashuhudia mengi sana ambayo leo hii kama ungetokea muujiza ukarudi tena huku ukashuhudia wewe mwenyewe kila kinachojiri, naamini ungeshangaa sana na yaliyo mengi pia ungeyakemea bila kumwogopa mtu yoyote, kama ilivyokuwa kawaida yako wakati wa uhai wako kukemea maovu bila kuogopa, pia katika kutetea wanyonge ungetetea sana, maana hali ni ngumu. Lakini pamoja na hayo bado kuna Amani na maraha tele telee...!!! katika nchi yetu hii iliyo jengwa nawe kwa misingi ya Ujamaa na kuimarishwa na mizizi ya haki na usawa kwa wote.
Pia jambo jingine ambalo nataka kukueleza Baba, kuwa; kwasasa unaongelewa huko Vaticani ili uweze kutangazwa kuwa Mwenye Heri ( Mtakatifu) na inawezekana ukawa Rais Mtakatifu wa kwanza kutangazwa hapa Duniani, si jambo dogo hili, yote haya ni heshima na busara zako ulizokuwa nazo katika uhai wako. Hii ni heshima kubwa sana kwako na kwetu sisi wanao Watanzania wa Taifa lako.
Utu wa mtu ni utu wake, nawe ulikuwa na utu kweli kweli hadi leo hii watu wengi Duniani wanakukumbuka na kukuheshimu, kwa utu uliokuwa nao. HESHIMA YA MTU NI UTU WAKE; SI MALI WALA CHEO, wakati wa uhai wako ulitamka mara nyingi maneno haya.
Mpendwa sana Baba wa Taifa! yote haya niliyo kuambia naamini umeyapata, najua kuwa hadi sasa Ulimwengu haujavumbua namna ya kuweza kuwasiliana moja kwa moja na watu muhimu wa namna yako, ambao Mungu alishawapenda zaidi kuliko sisi tulioko huku Duniani bado, lakini naamini vile vile kuwa kwa nguvu zake Muumba waweza kuzipata salamu zangu na zawatanzania wenzangu wote kwa ujumla, katika maadhimisho ya leo ya kukumbuka kifo chako.
Usishangae sana kwa stahili yangu hii ya kuwasiliana nawe, nia na madhumuni ni kuku kumbuka sana kwa mambo mengi mazuri uliyo yafanya na kuadhimisha miaka kumi na moja toka utuache hapa Duniani.
Mpendwa sana Baba wa Taifa! samahani naomba niishie hapa, kwasababu zipo habari nyingi sana za kukuhabarisha kwa hii miaka kumi na moja ambayo hupo nasi, lakini nafasi haitoshi, Mungu aendelee kukupa makazi mema huko ulipo. Mimi na Watanzania wenzangu wote tunakutakia mapumziko mema, nasi tutafuata huko ulipo ili tuje kuonana nawe katika siku, mwezi, mwaka, dakika, sekunde tusizo zifahamu.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YAKO BABA YETU WA TAIFA LETU; AMINA!





No comments:

WATEMBELEAJI