Tuesday, October 26, 2010

TANZANIA NAIPENDA SANA NA NADUMISHA AMANI NA MSHIKAMANO!

Tanzania; Utulivu na Amani ni siraha yetu, tudumishe Amani yetu tunu yetu njema. Tunu hii tumepewa kwa upendeleo...hatukuinunua kwa fedha tunu hii, bali Amani imetawala...Amani ni namba moja Tanzania.
Madaraka yasituchanganye, utajili usituchanganye, bali amani ni mhimu na ni namba moja kwa Tanzania. Tunapo kosoana wapendwa, tunapo elezana ukweli...Amani itawale daima! kwenye shida na kwenye furaha, kwenye njaa na kwenye huzuni...Amani itawale daima!
Tukumbuke ametupa bure, tukimwuzi ataiondoa Amani hii...tuitunze kama yai tunu hii njema ya Amani, tuilee na tuipambe vizuri tunu hii njema, tuitunze ili nayo itutunze, tuilishe na tuinyweshe daima kwa Utulivu na Amani sisi Watanzania hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.
IDUMU DAIMA AMANI TANZANIA.

-Mimi kila ninapopata wakati mgumu wa kutafakari, wanapotupeleka viongozi wetu, huwa natafuta solitude kwenye Amani waliotuachia Wazee wetu wa enzi za Mwalimu, Baba wa Taifa letu. Unajua Amani ni kila kitu, hata kama umezingirwa na mafisadi...lakini walau unapata wasaa wa kuburudisha roho yako ukiwa kwenye Amani yako.
Mwalimu Nyerere, Baba wa Taifa letu, alicheza sana aliposema; Ukabila uishie utani, dini iwe ni mapenzi ya mtu na nafsi yake. Maneno haya yametuweka hapa tulipo leo. Nasikitika tu generation ya watoto wetu, maana sisi Baba zao tunadhani Amani hii tuliyo nayo Mungu anaona aibu kutuondolea na kuwapa wenye akili na mapenzi nae.

MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE WOTE!

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

kwa kweli Tanzania tu- watulivu kweli na amani tunayo lakini je huu utulivu au ukimya wetu utatufikisha wapi?

Baraka Chibiriti said...

Inabidi tuanze kufumbuka macho na kuona kidogo kidogo...bila kwenda kwa kasi sana, maana tukija kwa kasi ndo vita vyenyewe vinapo tokea hapo.

WATEMBELEAJI