Wednesday, October 27, 2010

WAKATI WA THERUJI SASA UMEWADIA TENA KWA KASI!




Theruji/ Barafu sasa imewadia kwa kasi katika nchi nyingi za Ulaya, kwa hapa Italy mwaka huu imewahi, ila hapa niishipo bado haijashuka...tunaisikia na kuona kwenye TV. Hizi picha alinitumia rafiki wa huko Welsberg - Monguelfo, mpakani mwa Austria. Hii barabara nimeipita mara nyingi wakati nikienda huko kwao kuwasalimu, na hapo juu ni nyumba yao hao marafiki zangu. Nilipanga kwenda kuwasalimu hivi karibuni, sasa naanza kupata wasiwasi kwenda huko maana barabara mara nyingi hufungwa na huwa hatari sana kusafiri na gari wakati wa theruji, tabu za usafiri kwa Ulaya ni wakati huu.


No comments:

WATEMBELEAJI