Hapa ni mwezi Agosti mwaka huu, tukiwa Manyoni - Singida pamoja na wageni wangu wa kutoka Italy. Tukijiandaa kwenda safari ya Kijiji kinacho pika chumvi kwa wingi sana, kijiji kinaitwa Kinangali katika Wilaya ya Manyoni, Mkoani Singida. Katika kuwazungusha wageni hao kuona mazingira ya Tanzania, hasa vijijini ambako kuna maisha magumu sana! Kijiji hiko cha Kinangali kina utajili mkubwa sana wa chumvi, lakini hamna mtu yoyote au kingozi yoyote anaejali swala hili, hasa la kuwatafutia soko zuri hawa wananchi katia swala hili la chumvi. Tulioa jinsi wanavyo hangaka kuipika chumvi hiyo mpaka huzuni, na bado wanunuaji wanawakandamiza sana kwa bei ndogo ya kununulia chumvi hiyo. Huwa najiuliza sana katika maswala haya, lakini sipati jibu; mbona tuna utajili mkubwa sana nchini kwetu, tuna kila kitu lakini hamna anaefuatilia kabisa. Kijijini Kinangali wapikaji wachumvi walitupa maelezo, kuwa hawana soko kabisa ya chumvi hiyo nzuri kabisa, pia hufika wafanyabiashara kutoka nje ya nchi, kama Zambia, Malawi n.k, vile vile wakati tupo hapo tuliona Lori kutoka Zambia likipakia mzingo. Walisema kuwa wafanyabiashara hao wana walalia sana kwa kuwapa bei ndogo sana, kulingana na kazi wanayoifanya ngumu ya kupika chumvi hiyo, kutokana na kutokuwa na vifaa maalumu vya upikaji wa chumvi hiyo. Pia wafanyabiashara hao kutoka nje, wanasema kwao chumvi ni ya shida sana, mpaka inawaladhimu kufuata Tanzania. Mimi niliwauliza wana kijiji hao kama wamewahi kujaribu kuongea na baadhi ya vingozi ili waweze kusaidiwa kutafutiwa masoko na vifaa vyakutengenezea chumvi hiyo; walisema wamefikisha maombi mbalimbali kwa viongozi mbalimbali, lakini wanawajibu hawana mda huo, hivi viongozi wetu ni viongozi wetu au?
Wageni wangu walisikitika sana kuona mali kubwa kama hiyo ya chumvi tuliyo nayo Tanzania, haichukuliwi umhimu wowote. Akina mama na watoto wanahangaika tu, katika kupika chumvi hiyo.
Basi niishie hapa, lakini nitaendelea kuwaleteeni picha zaidi za Kijiji hicho cha Kinangali, na ili tuone zaidi jinsi wanavyo pika chumvi hiyo.........
No comments:
Post a Comment