ASKOFU RUWAICHI ATEULIWA KUWA ASKOFU MKUU WA JIMBO KUU LA MWANZA - TANZANIA.
Baba mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemteua Askofu Yuda Thaddeus Ruwaichi, wa jimbo katoliki la Dodoma kuwa Askofu mkuu wa jimbo kuu la Mwanza. Askofu mkuu mteule Ruwaichi pia ni Rais wa Baraza la maaskofu katoliki Tanzania. Askofu mkuu mteule alizaliwa tarehe 30 Desemba 1953, Parokia ya Kilema, Jimbo katoliki la Moshi.
Akapadrishwa kunako tarehe 25 Novemba 1981. Tarehe 16 Mei 1999 akasimikwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbulu. Tarehe 15 Januari 2005 akateuliwa kuwa Askofu na hayati Baba mtakatifu Yohani Paulo wa pili, kuwa Askofu wa Jimbo katoliki la Dodoma na kusimikwa tarehe 19 Februari 2005, kwenye kanisa kuu la Mtakatifu Paulo wa msalaba, Jimbo katoliki Dodoma.
Askofu mkuu Ruwaichi anachukua nafasi iliyoachwa wazi baada ya kifo cha marehemu Askofu mkuu Anthony Mayala, wa Jimbo kuu la Mwanza, kilichotokea tarehe 19 Agosti 2009.
-Kila lakheri Baba Ruwaichi huko uendako Mwanza, tulikuzoea sana Dodoma sisi wana wa Idodomia....lakini basi ndo mipango ya uchungaji wa kanisa hii.
No comments:
Post a Comment