Wednesday, November 10, 2010

BAA LA UMASKINI TANZANIA NI PENGO KATI YA MASKINI NA....

BAA LA UMASKINI TANZANIA NI PENGO KUBWA KATI YA MASKINI NA TAJIRI LINATISHA!

Serikali ya Tanzania imepiga hatua kubwa katika kupambana na baa la Umaskini kati ya Wananchi wake kwa kuboresha elimu, afya na huduma za kiuchumi na kijamii. Lakini jambo linalosikitisha ni pengo linalozidi kuongezeka kati ya maskini na matajiri, kati ya watu wanaoishi mijini na wakulima vijijini. Maendeleo ya vitu yamepewa msukumo wa pekee, lakini Utu na Heshima ya Mwanadamu bado vinasua sua, mtu Tanzania anathaminiwa kwa vitu anavyomiliki na wala si kwa Utu wake. Tabia hii imekua sana kwasasa, hasa mijini....ambapo zamani haikua hivi kabisa, matokeo yake ni kundi kubwa la vijana kukimbilia mijini wakati wakiwa na ndoto ya kutaka kuboresha hali yao ya kimaisha.
Hali duni ya wakulima vijijini itoe changamoto kwa wadau mbalimbali wa maendeleo nchini Tanzania. Tukiangalia tatizo la umaskini na kutoa angalisho kwamba; ikiwa kama hali ya wananchi wanaoishi vijijini haitainuliwa kwa njia ya haki, kuna hatari ya Amani na Utulivu kutoweka kwani watu wakisha lamba asali, watataka kuchonga mzinga. Wameona maendeleo ya vitu mjini, wasipokuwa na njia halali ya kukidhi mahitaji yao, mapambano ya rushwa, ubadhirifu wa mali ya umma, wizi na ufisadi vitaendelea kuwa ni tenzi na porojo za kisiasa kila kukicha.

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Kaka umenena ni kweli vija wengi wanakimbilia mjini na wanafikiri huko ndiko kuna maisha bora. Na sasa inabidi tufanye haraka ili kuelimishana kuwa maisha ni kujituma huwezi kupata maisha bora bila kufanya kazi, kwani hata mjini utafanya kazi. Na kuendelea si lazima mtu awe na mtaji mkubwa ili kuondoa umaskini......

WATEMBELEAJI