Monday, November 22, 2010

BWAWA LA MTERA - UKIWA UMETOKA DODOMA KWENDA IRINGA!

Barabara ya kati ya Dodoma to Iringa, unapitia vijiji vingi kati ya hivyo unakutana na Mtera ambapo kuna Bwawa zuri ambalo linagawa pia umeme nchini kwetu. Barabara hii nimeipita mara nyingi sana kwenda katika Kijiji cha Migoli hadi Iringa. Migoli mara nyingi tulichimba visima vya maji katika Misheni ya Migoli na vijiji vya karibu. Pia nimetumia barabara hii kwenda Iringa hadi Makalala, nilipo ona picha hii kwa mkuu Mjengwa nilifurahi sana na kukumbuka mengi.

-Picha na Maggid Mjengwa.

No comments:

WATEMBELEAJI